JIFUNZE MAANA YA VITU HIVI MUHIMU KUHUSU LAPTOP KABLA HUJANUNUA

        Karibuni ndugu wasomaji wa blog hii pendwa na leo tutakwenda kupata ufahamu kuhusu Laptops au kompyuta mpakato, Nimeamua kupost kuhusu swala hili kwani watu wengi huwa wanapata usumbufu pale wanapotaka kununua laptop kwaajili ya matumizi mbali mbali,
   Sasa nitatoa magroup tofauti ya watumiaji na pia kila group nitatoa mapendekezo mbalimbali ya sifa gani za laptop zinazotakiwa katika group hilo,

Matumizi ya Laptop

  Mpaka mwaka huu 2017 watu wengi wamekuwa wakimiliki aina mbalimbali za laptop ila "JINA" la kampuni sio kitu ambacho ninaweza kusema cha kuangalia wakati wa uchaguzi wa laptop mfano; mtu anaweza kusema "ninapenda laptops za HP sababu ni nzuri sana na zina dumu", ni kweli inawezekana kilicho semwa ni cha kweli lakini tunapokosea wengi ni kwamba tuna toa experience ya kampuni fulan bila kufuatilia  ni wapi walipokosea, HP wana Product line za laptop zinaitwa Pavilion, Envy, Compaq,Elitebook,Probook,Omnibook nk. kwahiyo mfano Specs na kila aina ya hardware itakayowekwa kwenye  Compaq haiwezi kulingana na itakayo kuwepo kwenye Envy na kadhalika, hii ni kwasababu kila aina ya productLine inayo tolewa na HP inatolewa kwa maksudi maalum tukiangalia Laptops zenye jina la Compaq zimetolewa kwa matumizi ya ofisini yale ya kupanga documents na kadharika  ndio maana wanaziita Business Laptops, natumaini umepata point yangu ninayo taka kuzungumzia kwahiyo ukinunua laptop ya Compaq ukategemea kwaajili ya mambo ya kucheza games na kutumia software kama photoshop utakuwa umekosea na lazima ikusumbue na mwisho wa siku lazima useme ni mbaya nzito na kadhalika,


AINA ZA LAPTOP

  Laptop zipo nyingi na kadha wa kadha  katika kipengele hiki sitowapa aina ya laptop kufuata mtiririko wa kampuni (HP,DELL,ASUS nk) bali nitatoa aina na kuiweka katika group  kutokana na ufanyaji kazi wake kama ifuatavyo


  • GAMING LAPTOPS
  • CASUAL LAPTOPS/BUSINESS LAPTOPS
  • MOBILE WORKSTATIONS LAPTOPS
 
  GAMING LAPTOPS 
  Kwa wanaopenda kucheza game mbalimbali katika laptops zao hii ndio sehemu yao,hata laptop zilizo katika kundi hili pia zimegawanyika katika makundi matatu kutokana na utafiti wangu,

kundi la kwanza ni Low End Gaming Laptop

 Hizi ni zile naweza kuziweka katika group hili lakini nguvu yake ya kuweza kucheza games ni ndogo kwahiyo hapa utacheza games za miaka ya nyuma mpaka 2015 na kidogo za 2016 ambazo pia baadhi za games utalazimika kucheza katika lowest settings  kama unavyoona hapo chini katika picha.
               

   Laptops ambazo unaweza kucheza games ni nyingi na sio lazima ziitwe gaming laptop lakini katika kundi hili tunaongelea zile ambazo zimetengenezwa kwaajili ya kucheza games

 kundi la Low end ambazo pia ni zinapatikana kwa bei nafuu ambazo unaweza kununua zitakuwa na specs kama ifuatavyo

HDD(Hard Disc Drive) - Kuanzia 500GB na kuendelea (kama utapata inayo support HDD mbili unaweza kuweka SSD (Solid State Drive)  nitaelezea maana ya SSD mbele katika post hii)

RAM - GB 4 na kuendelea
GPU -   AMD Radeon series 4000 kwenda juu ( Video card memory GB 1 DDR3  kwenda juu) au Nvidia GeForce GTS 250 kwenda juu (Video card memory GB 1 DDR 3   kwenda juu )
CPU -  Intel core i5 atleast ianzie Second generation (Yenye 3 MB Cache 2.40Ghz  ) au kama ni mpenzi wa processor za AMD basi iwe A series na atleast ianzie A6-5200 ( yenye 2MB Cache 2Ghz na kuendelea )

  Kuna utofauti mkubwa sana katika processor za AMD na zile za Intel na pia kwa kawaida processor za intel zina uwezo mkubwa kuliko zile za Amd  kwahiyo hapa ninge washauri watu wachague laptops zenye processor za intel, nita post topic inayo jitegemea kuhusu processor ila kwa sasa  tembelea website ya Intel hapa ukajifunze zaidi  AMD na INTEL  

   Kwa upande wa HDD nimechagua 500GB kwasababu naamini kwa kiasi games zitakazo cheza katika uwezo huu zitakuwa zina around GB 10 mpaka 30 kwahiyo nadhani ni nafasi inayotosha hata ukiwega games 10, na swala la SSD ni zuri na pia kwasababu zina uwezo wa kupeleka na kurudisha data kwa haraka zaidi kuliko HDD, kwahiyo ukiona umepewa laptop wakakuambia ina SSD ichukuwe bila hofu hata kama ina 60GB kikubwa cha kuangalia kama ina nafasi ya nyongeza ya kuweka HDD kwasababu inashauriwa uki install OS (wengi wanaita window) kama una SSD nivizuri uchague ku install huko alafu maswala mengine ndo HDD
   GPU ni kitu muhimu sana katika swala la wacheza games na kama unataka GPU nzuri vilevile uchague ya nVidia na usinielewe vibaya kwakweli, sio kwamba AMD sio nzuri hapana ni kwamba tu nVidia wako vizuri sana, kwa mfano mimi natumia AMD kwenye PC yangu na sio siri ni very powerful nimeweza kucheza game hadi la Call of duty Advanced walfare (ingia hapa ulicheki ), Middle earth shadow of mordor(ingia hapa ulicheki), The witcher 3 (ingia hapa ulicheki), PES 2017 na kadhalika lakini bado tukiringanisha GPU ninayotumia ambayo ni AMD na nikachukua moja kutoka nVidia ambazo zote zipo kwenye level moja na bado yangu ina GB 2 na NVidia ina GB1 basi NVidia  na yakwangu zinatoa droo ona HAPA
   
  Kwa kumaliza ningetoa mapendekezo ya laptop gani inayo fit katika kundi hili unayoweza kununua iwe hapa nchini au nje ya nchi kama  vile Ebay au Amazon


  •  HP-EliteBook 8460p  
     



CPU-  Core i5 520M 2.40

GPU- ATI/AMD Radeon HD 6470M - 1GB DDR3
RAM- 4GB
HDD-500GB
BEI - Unaweza kupata kwa Tsh 400,000 ukinunua Ebay au Amazon kwa hapa Tz inategemea na dukani ila Bei yake inaweza kuanzia Tsh 600,000(bei inaweza kupanda).




  • Toshiba Satellite L655-PSK1LE
 




CPU-  Core i5 460M 2.53

GPU- ATI/AMD Radeon HD 5000 series - 1GB DDR3
RAM- 6GB
HDD-500GB
BEI- Kama utaipata hapa Bongo unaweza kununua kwa Tsh 900,000 (bei inaweza kupanda) ila kama utanunua Ebay unaweza kupata kwa Tsh 600,000




  • Dell-Latitude-3540

   



CPU-  Core i5 520M 2.40

GPU- Intel HD Graphics 4400
RAM- 4GB
HDD-500GB
BEI- Bei ya hii unaweza kununua kwa Tsh 600,000 Ebay lakini Tz hapa unaweza kuipata kwa Tzsh 1,000,000




  •  Asus N61j series





CPU-  Intel Core i5 520M 2.40

GPU- ATI/AMD Radeon HD 5000 series - 1GB DDR
RAM- 4GB
HDD-500GB
BEI- Sidhani kama bongo zinapatikana hizi ila kama ukiipata utaweza kununua kwa Tsh 900,000(bei inaweza kupanda) ila ukinunua sehemu kama Ebay unaweza kuapata kwa Tzsh 400,000


  Kwa hizo nne ni baadhi ya laptop ambazo unaweza kuzinunua na ukafurahia, ila sio kwamba ndio hizo tu, bali ziko nyingi mno lakini kitokana na hizo specs natumaini unaweza kupata chaguo nyinginezo



Kundi la pili ni  Mid End Gaming Laptops




     Hapa Ndipo zinapatikana zile laptops zinazo cheza games with medium settings, ambazo kwa namna moja au nyingine huwa siwashauri watu wanunue yani ni bora utoke Low kwenda High aina ulazimu wakupitia hapa labda kama mfuko hauruhusu na unahitaji kwa uharaka, ila kama hauna haraka unaweza kusave ili uweze kununua High End.

  Specs zinazohitajika katika kundi hili ni kama zifuatazo;

   HDD(Hard Disc Drive) - Kuanzia 500GB na kuendelea (kama utapata inayo support HDD mbili unaweza kuweka SSD (Solid State Drive)  )

RAM - GB 6 na kuendelea (kama laptop yako ina support sehemu mbili za kuweka ram unaweza ukaweka nne x mbili na ukapata Gb 8)
GPU -   AMD Radeon HD 6970M  kwenda juu ( Video card memory GB 2 GDDR3 Kwenda juu ) au Nvidia GeForce GTX 645 kwenda juu (Video card memory GB 2 GDDR 3 kwenda kwenda juu )
CPU -  Intel core i5 atleast ianzie 3rd au 4th generation (Yenye 3 MB Cache 2.80Ghz na kuendelea(turbo)  )  ) au AMD processor kuanzia Series A8 kwenda juu (3MB Cache 2GHz kwnda juu)

   Tujifunze kwa ufupi wala usiangalie ukubwa wa memory zinazo patikana katika GPU (GB1 au 2 au 4 nk) kwasababu hizo sizo zinazo sababisha performance iwe nzuri katika laptop haswa kwa upande wa GPU  kikubwa kinacho sababisha mpaka GPU iwe nzuri ni clock frequency(sijui nisemaje kwa kiswaili) na Aina ya Chip inayokuwa katika GPU, katika games kuna njia nyingi za kuweza kupima uwezo wa GPU na kwa kuweza kufananisha  na mara nyingi NVidia wamekuwa wakiinuka kinara, mfano; AMD wana GPU  yenye Vram yenye 4GB iitwayo Radeon R7 M270  na ukichukua moja kutoka nVidia ambayo iko kwenye level hiyohiyo iitwayo GeForce GTX 680MX yenye 2GB utaona kwamba hii ya NVdia ndiyo ina nguvu zaidi kuliko hiyo yenye 4GB kutoka AMD.


  Katika group hili ningeweza kutoa ushauri wa laptop za kununua kama ifuatavyo;




  • Dell Inspiron 15R 7520
  

CPU-   Intel Core i5-3210M

GPU- Radeon HD 7730M + Intel HD4000 2GB GDDR5
RAM- 6GB
HDD-500GB
BEI- Inapatikana kwa Tzsh 700,000 kama utanunua Online kwa hapa Tz kama utaipata itakuwa kwa Tzsh 1.2m



  • MSI GX60





CPU-   Quad-core A10-5750 Processor

GPU- Radeon HD 7970M 2GB GDDR5
RAM- 8GB DDR3
HDD-1TB(500GB x 2)
BEI- Kama utanunua Online unaweza kununua kwa Tzsh  750,000 ila kwa hapa Tz mimi  sijawai kuziona ingawa nishamuona mtu ana miliki lakini kama itakuwepo utaweza kununua kwa Tzsh 1.5M(bei yaweza kupanda)




  • Asus G74SX ROG


CPU-   Quad-core A10-5750 Processor
GPU- GeForce 560m 1.5GB GDDR5
RAM- 8GB DDR3
HDD-500GB
BEI-Bei yake kwa online unaweza kupata kwa Tzsh 850,000 hapa bongo hakuna soko kwa sana ila kama utapata itacheza kwenye Tzsh 1.6M(bei inaweza kupanda au kushuka)




  • Toshiba Satellite L50-B-1X4

CPU-   Intel Core i5 4th Gen
GPU- AMD Radeon 7 M260 2GB GDDR5
RAM- 8GB DDR3
HDD-500GB
BEI- Kwa bei ya hii laptop Online unaweza kulipia Tzsh 700,000 lakini kama utafanikiwa kununua hapa Tz utapata kwa Tzsh 1,000,000 (Bei inaweza kupanda)




  Sasa hizo ni baadhi ya laptop ambazo unaweza kununua na ukafurahia kwa kucheza games hata kwa ku run software za ku edit kama vile photoshop na kadharika ingawa GPU yake haiku designiwa kwa ajili hiyo,  kama una swali lolote unaweza kuniuliza chini katika comment.



Kundi linguine na la mwisho ni  High End Gaming Laptop

  Sasa tukizungumzia High end  naomba usikosee kuelewa, ni kwamba High end inaweza kufanya kazi yeyote ikiwemo video production mpaka 4k(Premier pro, After effects, sony vegas nk) kama mzee wa ku edit  na nini unaweza kutumia hizi laptop ila tu unatakiwa uelewe kwamba haziku tengenezwa kwa ajili hiyo kwahiyo GPU zinakuwa na uwezo tofauti na matumizi, Kingine ningependa kuwakumbusha ni kwamba unaweza ukawa na laptop yenye power ya kutosha lakini siku zote haziwezi kufikia Desktop (yenye Tower) tena zile ambazo ni custom made, Na pia hapa  nita base kwenye Specs na Bei ya laptop(3 za bei nafuu na 3 za bei ya juu) na muonekano, nitakuja kuelezea umuhimu wa kutengeneza Desktop mwenyewe kwa kupachika vifaa mbali mbali kwenye post nyingine kwa sasa twende tukaangalie hizo laptop

kingine hapa cha tofauti ili uweze ku enjoy game katika High settings ni lazima display iwe nzuri na hapa nitazichagua kutokana kuweka uwezo wake wa display ikiwemo Resolution, Quality, na kadharika


list hii ni randomly sijapanga ipi inauwezo Zaidi sijui na blah blah blah

Naanza na zilizo bei nafuu ila ni the Best. (Powerful rate 89%)



  • Dell Inspiron 7559


CPU-   Intel Core i7 6th Gen
GPU- NVIDIA GeForce GTX 960M 4GB GDDR5
RAM- 8GB DDR3
HDD-1TB(500GB x 2)
RESOLUTION -  FHD (1920 x 1080)
BEI - Gharama ya hii Laptop kwa Online ni Tzsh 1.5M  kama utanunua hapa Tz andaa 2M ( Tena Bei inaweza kupanda)




  • MSI GL62M
    
CPU-  Intel Core i5-7300HQ 7th Gen  2.5 GHz(Turbo 3.1Ghz)
GPU- NVIDIA GeForce GTX1050Ti 4G GDDR5
RAM- 8GB DDR4 2400MHz
HDD-1TB(500GB x 2)


RESOLUTION -  FHD (1920 x 1080)
BEI - Online hii unaweza kupata kwa Tzsh 1.9M




  • Lenovo Y700



 CPU-   Intel Core i7 6th Gen

GPU- NVIDIA GeForce GTX 960M 4GB GDDR5
RAM- 16GB DDR3
HDD-1TB(500GB x 2) 
RESOLUTION -  FHD (1920 x 1080)
 BEI - Haya Sasa.. Hii kama mfuko uko poa unaweza kupata Online kwa Tzsh 1.4M hapa Tz kwakweli mmhh..


  Sasa hizo nilizoonyesha hapo juu ni nzuri sana na zina nguvu sana tu, lakini angalau bei yake inaweza kununulika bila shida (Kama unapesa) zifuatazo ni baadhi ya powerfull bila kuangalia bei najua pia zitanunulika na wale wapenzi


Hapa hatutaangalia bei tutaangalia perfomance,display na Muonekano.





  • MSI GS Series GS43VR PHANTOM PRO-069



CPU- Intel Core i7 7th Gen 7700HQ 2.80 GHz (Turbo 3.5Ghz)

GPU- NVIDIA GeForce GTX 1060 6GB DDR5
RAM- 16GB DDR4
HDD-2 TB HDD + 512 GB SSD
RESOLUTION - 4K (3840 x 2160)
BEI- Online utaweza kununua kwa Tzsh 2.5M



  • Alienware 15 R3
 



CPU- Intel Core i7 (7th Gen) 7820HK / 2.9 GHz (Turbo 3.9Ghz)

GPU- NVIDIA GeForce GTX 1060 8GB DDR5
RAM- 16GB DDR4
HDD-1 TB HDD + 512 GB SSD
RESOLUTION - FHD (1920 x 1080)
BEI - Kama utafanikiwa kununua Laptop hii utaweza kununua Online kwa Tzsh 4M




  • The Razer Blade




CPU- Intel Core i7 (7th Gen) 7700HQ / 2.8 GHz (Turbo 3.8Ghz)

GPU- NVIDIA GeForce GTX 1060 6GB DDR5
RAM- 16GB DDR4
HDD-1 TB SSD + 512 GB SSD
RESOLUTION - 4K (3840 x 2160)
BEI- Haya Hapa utanunua kwa Tzsh 3.8M




  Kwa hizo laptop zote hapo juu kwanza kabisa, kama ingekuwa ni chaguo basi mimi ningechagua

Alienware 15 R3 kwasababu ya muonekano wake na mengine ni mbwembwe tu zilizo wekwa katika hiyo Laptop,
   Kwa kufunga na hili group naweza kusema kwa bei hizi za mwishoni kabisa naweza kusema bora mtu ununue low end Gaming alaf swala la ku game kwenye high end ni bora utengeneze Desktop kwa kutumia vifaa mbalimbali na kwa bei hiyo hiyo na unaweza kupata yenye nguvu kuliko hiyo laptop.
 


 CASUAL LAPTOPS/BUSINESS LAPTOPS


    Hizi ni laptop ambazo kama nilivyosema hapo juu kuwa ni kwa wale wenye matumizi ya kawaida  kama ya kiofisi na mengineo kama kuangalia movies na kadharika, Hapa sitatoa kutenganisha kwasababu hakuna moja inayo mzidi mwenzie kwasababu zipo kwaajili ya matumizi ambayo yote yana lingana, sana sana wengine wanapenda kutumia kutokana na muonekano na maurembo kadha wa kadha.


 Specs utakazo hitaji hapa ni kama vile :


  HDD- Kuanzia GB 320 na kuendelea

  RAM- GB 2 na kuendelea
  CPU- Angalau uwe na core i3 1st Gen (unaweza ukawa na core2duo ambayo nayo si mbaya)
  GPU- Integrated (Sio lazima uwe na GPU ambayo ni dedicated kama hizo za juu )

 

   Twene niwape mifano ya laptop ambazo unazweza kununua kwa matumizi yako ya kawaida, na hata kama hautapenda nitakazoziweka hapa basi unatakiwa kujitahidi kufannanisha specs ambazo nadhani ndio standard



  • Lenovo-ThinkPad-T420


CPU- Intel Core i5 2.50Ghz 1st Gen
GPU- Integrated/On-Board Graphics
RAM- 4GB DDR3
HDD-320GB
BEI - Hapa kama unataka hii ukinunua Online unaweza kupata kwa Tzsh 250,000 tu, kwa hapa Tanzania unaweza kupata kwa Tzsh 500,000




  • HP ProBook 6570b




CPU- Intel Core i5 2.50Ghz 2nd Gen

GPU- Intel HD Graphics 4000
RAM- 4GB
HDD-500GB///
BEI - Hapa kama unataka hii ukinunua Online unaweza kupata kwa Tzsh 270,000 tu, kwa hapa Tanzania unaweza kupata kwa Tzsh 500,000






  • ASUS UL30Vt




CPU- Intel Core2Duo

GPU- Intel® GMA X4500MHD & NVIDIA® GeForce® G 210M 512MB
RAM- 4GB
HDD-500GB
BEI -  kama unataka hii ukinunua Online unaweza kupata kwa Tzsh 350,000 tu, kwa hapa Tanzania unaweza kupata kwa Tzsh 600,000



    Basi ndugu wasomaji hiyo ni baadhi ya mifano ya laptop ambayo wengi najua huwa wanachanganya sana ifikapo wakati wa kuchagua laptop kwani wengi wana danganywa na muonekano na mwisho wa siku wana shindwa kutimiza aja zao.






  MOBILE WORKSTATIONS LAPTOPS

  Katika kundi hili laptop ambazo nitazitaja ndizo ambazo wale watu wanaopendelea maswala ya Editing na kutuia Video production,wakutumia CAD na maswala ya Engineering ku design majengo, 3D paints na kadharika, kwa maswala ya mziki  kuedit  au kutengeneza Beats  mambo ya uDj  na mengine kibao basi hizi laptop hapa ndizo zinawafaaa, bila kuchelewa twende kwenye  list yetu!



   Katika list hii tuta tizama bei na ubora na ukaaji wa chaji, kwani nafahamu watu huweza kufanya kazi zao za production hata wakati umeme umekatika (TANESKOOO!!)  au safarini au katika location kwa wazee wa video production.

  Ifahamike  na hapa kwamba sio kwamba laptop inaweza kukidhi mahitaji yako yote kama kweli umejikita kwenye production tumi Desktop mzee!!! laptop ni temporally workstation.

     Kama utahitaji workstation basi unaweza na specs kama zifuatazo kwa wale watumiaji wa kawaida  na  wale wa hali ya juu (Heavy power users) lakini pia tunaangalia na matumizi ya umeme je ni kiasi gani zitahitaji umeme na zitakaa nao kwa muda gani?

 
      GPU- Hapa ni muimu sana tena sana kufahamu ni GPU gani utahitaji kwa hapa GPU tunazo hitaji ni kama ifuatavyo, kama unapenda AMD basi chagua zinazoitwa  AMD Fire Pro na kwa wale wenzetu wa NVidia kama uangalie GPU ziitwazo  NVidia Quadro
   kwa kuanza  NVidia ya chini kabisa ningependa niwashauri uanze na GPU iitwayo K1100M ambayo ina GB2 GDDR5  Na kwa wale wanaotumia AMD unaweza kuanza na AMD FirePro M2000  GDDR5 1GB.



   



  •  Dell-Precision-M6600
  



CPU- Intel i7 2720QM 2.20 GHz (3.0Ghz)

GPU- NVIDIA Quadro 3000M
RAM- 8GB
HDD-500GB
BEI -  kama unataka hii ukinunua Online unaweza kupata kwa Tzsh 600,000 tu, kwa hapa Tanzania unaweza kupata kwa Tzsh 1M





  • DELL PRECISION M3800
    

CPU- Intel Core i7-4702HQ 2.2Ghz

GPU- Nvidia Quadro K1100M 2GB
RAM- 16GB
HDD-512 SSD
BEI -  kama unataka hii ukinunua Online unaweza kupata kwa Tzsh 1.2M tu, kwa hapa Tanzania Unapigwa parefu tu.




  •  HP-ZBook-15-G3
  


CPU- Intel Core i7-6820HQ 6th Gen 2.6Ghz (Turbo 3.6Ghz)

GPU- NVIDIA Quadro M1000M 2GB GDDR5
RAM- 8 GB DDR4
HDD-1TB + 256 SSD
BEI -  kama unataka hii ukinunua Online unaweza kupata kwa Tzsh 2M tu, kwa hapa Tanzania Utajuta kununua (si kwa bei hiyo)



  • MSI WT72 6QM



CPU- Xeon E3-1505M v5 2.8 GHz (3.8Ghz)

GPU- NVIDIA Quadro M5000M 8GB GDDR5
RAM- 32 GB
HDD-1TB + 256 SSD
BEI -  kama unataka hii ukinunua Online unaweza kupata kwa Tzsh 5.5M tu, kwa hapa Tanzania Utajuta kununua (si kwa bei hiyo)



 MAWAZO BINAFSI




    Nimetoa aina tofauti hapo juu kutoka ya bei nafuu mpaka bei ya bei ya kununua gari,  la kini mwisho wa siku wewe ndiye ambaye utaangalia mfuko wako unasemaji lakini kwa sasa nadhani kidogo utakuwa umepata idea fulani kabla ya kwenda kununua laptop bila kufahamu ni ipi unayoitaka.

   Kingine labda naweza kuongezea hapa ni kwamba mimi nadhani laptop za Mac ni nzuri mno sawa lakini tunapokuja kwenye swala la ku customize baadhi ya vitu haswa kwa High Laptops Mac ndipo wanapo fail na siku zote kitu ambacho unaweza kutumia leo na kesho ukaweza ku upgrade ni kitu kizuri sana na ndio maan sijawaweka katika list ila kama ni mpenzi wa Mac unaweza kununua haswa kwa wale wa Maswala ya production kwani in perfom vizuri sana kwenye swala hilo ila kwenye Games baki na kompyuta zinazokuwa na windows! na kwa wale wa Casual unaweza kutumia Macbook kwanza kwaajili ya muonekano na upekee na Quality itafaa sana sema tu nao kwenye swala la bei ndipo wanapo chosha watu wengi haswa sisi wa TZ,
     Kuna mambo mengi ambayo pia sija  yaongelea kwasababu naona kwama hayana umuhimu sana pindi ununuapo laptop lakini pia sio vibaya ukayafahamu kwasababu yanaweza kusaidia kwenye shughuri moja au nyingine Mfano: USB 3.0 hii ni feature ambayo inapatikana katika laptops na mara nyingi ukiangalia laptop katika port ya kuchomeka USB utaona kuna rangi ya blue basi hiyo ndiyo USB 3.0 na kazi yake kubwa ni ku transfer data kwa ufasta sana tofauti na za kawaida ambazo ni 2.0, mengine ni kama thunderbolt,Aina ya HDD(5400 au 7200Rpm) , Trackpad,HDMI, Mlango wa DVD, Keyboard , port mbali mbali OS kiujumla, Webcam, Spika (kuna zenye subwoofer) , ukaaji wa betri na mengineyo . Kwahiyo lengo la hii post ni kufahamu kwanza alaf mbeleni nadhan nitaposti mambo mbali mbali yanayo tuzunguka katika laptops zetu ili iwe rahisi kutumia.



Asanteni sana na karibuni kwa post nyingine



Cheers..

Post a Comment

4 Comments

  1. Asante kwa ushauri wako mtaalamu wetu mimi Nina hp 2000 inaweza kufaa? Kama haifai naweza kuiboresha?

    ReplyDelete
  2. Asante sana kwa swali lako, kabla hatujakwenda mbali unaweza kunitajia specs za kompyuta yako (ram, cpu hdd nk..) alaf pia naweza kujua unatumia kwa matumizi gani haswa?

    ReplyDelete
  3. Kwanza kabisa nasema ahsante kwa darasa nililopata kwa maana siku zote nilikuwa siyafahamu ayo, hila maoni yangu ni kwamba umesema kuna Gaming laptop sio kana kwamba uwezi kufanyia shughuli zengine kama za ki office kam vile Word, Excel nk Au unuweza ukafanyia?

    ReplyDelete