
Habari ndugu wasomaji wa blog hii pendwa kabisa na leo tutaenda kuelewa kitu tofauti kabisa na tulivyo zoea, Swala la tv ndugu zangu limekuwa ni muhimu katika maisha yetu sote kw matumizi mbalimbali lakini je? ushawahi kufikiria Tv gani ambayo ingekufaa au kukuridhisha?
Kwanza kabisa tufahamu tupo mwaka 2017 na teknolojia imebadilika kwa kiasi kikubwa na watu wanaamia kwenye ulimwengu wa flat panel ( maarufu kama flat screen) kama kuna watu wenye zile za zamani A.K.A vichogo basi naamini ni wachache ambao watakuwa wanasoma post hii kama wapo mmmhhhh, basi bila kupoteza muda twende kwenye maelezo zaidi..
TV GANI UNATAKIWA KUNUNUA
Kuna makampuni mengi hivi sasa yanayo tengeneza aina mbali mbalimbali za Tv kama vile Samsung, LG, Hisense, Sharp , TLC, Philips na kadharika... Kila kampuni ina aina yake ya utengenezaji wa bidhaa zao na sifa zxa kipekee ila sote tunatambua kuwa LG, SONY na Samsung ndio wameliteka soko la Tv kwa sasa ingawa unaweza kupata Tv nzuri kutoka katika makampuni mengine bila shaka lolote, kwa hiyo kwa kujibu swali hili ningeweza kukujibu kwa kusema kwamba usiangalie kampuni ili ununue TV nzuri bali angalia budget uliyo nayo + ubora wa bidhaa + size ya kioo ukipendacho, kwa mfano:- mimi nina kaki tano (500,000 Tzsh) nataka nipate flat iliyo smart ambayo pia ni inch 32, sasa tukiangalia katika makampuni kama SONY au LG au Samsung kamwe kupata TV ya namna hiyo hutoweza kupata labda iwe used. ila ukichukua uamuzi wa kutembelea makampuni mengine unaweza walau kupata tv kama hiyo kwa mfano Sharp au TLC, kwahiyo mwisho wa siku nafaham wengine hawawezi kutumia kitu kutoka tofauti na kampuni flani kwasababu pengine wanaona kuwa labda ndio zina dumu nk. kitu hicho si cha kweli na labda tu niwafahamishe kuwa makampuni yote yanafanya biashara na mara nyingi makampuni makubwa huwa wana toa bidhaa zenye bei kubwa huku wakiongeza kiyu kidogo tu katika bidhaa yao, kwahiyo chakufanya ni kuangalia ni sifa gani unazo taka kwaajili ya Tv yako ili uweze kuridhika bila kugharamia pesa nyingi ila kama una hela braza unamwaga tu hiyo mipesa. :p
FAHAMU RESOLUTION GANI ITAKUFAA KATIKA TV
Resolution ni swala muhimu sana katika TV na ninaamini watu wengi sana huwa hawafuatilii swala hili na baadhi yetu sidhan kama tunafahamu hata maana yake, sasa kama ushawai kupita dukani ukaulizia Tv basi lazima watakuambia "Hii ni HD" sasa watu wanafahamu kuwa HD ni kwamba Quality ya picha katika Tv yako ni nzuri well ni kweli lakini hizohizo HD hua zinatofautiana , nita orodhesha kama ifuatavyo:-
HD
Ukiona HD huwa inawakilishwa na 1280x720 pixels au huitwa 720p (soma hapa kuelewa maana ya Pixels) na hii sasa ndio ile ukienda kaliakoo watakuambia hi ni HD hii ni HD lakina hawatoi maelezo yakutosha sasa ngoja niwaonyeshe utofauti wake
Ningekuwa nimeweka HD pekeyake usingeweza kutofautisha lakini ukiangalia hapo uta ona kiji utofauti kidogo hapo na hiyo ndio maana ya pixels na umuhimu wake katika Tv unapata kitu chenye detals nzuri. Lakini mwisho wa siku HD iko poa ila tu ukiamia daraja linalo fuata uataona HD ilikua ya kawaida tu.
FULLHD (FHD) - Hii sasa inawakilishwa na 1920x1080 Pixels maarufu kama 1080P unaweza ukapita kwa sasa kwenye baadhi ya maduka ukakuta stika zimebandikwa kwenye baadhi ya TV ukitizama utaona kimeandikwa (FHD) lakini pia wauzaji wengi huwa hawaelezei utofauti wake , kwa ufufpi hii ndio wengi wanatakiwa wawe nayo kama ukitaka uzuri wa content katika Tv yako ingawa kuna 4K lakini kiukweli kiTz bado sana angalia picha hapa chini:-
Kama uanavyo hapo picha za 4k zina details kwa wingi na ziko very sharp lakini still hauwezi kusema kuwa 1080P ni mbaya iko very good na inaonyesha vizuri sema 4k ni vizuri zaidi
4K - Hii inawakilishwa na 3840 × 2160 Pixels maarufu kama 4K sikuizi watu wengi wengi wana ziongelea lakini naamini uwelewa ni mdogo juu ya hili swala kwasababu kwanza Tangu mwaka 2015 mapinduzi ya 4k yalipoingia kwa wale watu wafuatiliaji wa Dunia ya kiteknolojia contents nyingi kama vile movies music videos etc zinapatikana kwenye 1080p kwa sana na baadhi ambazo nimeziona zinapatikana ni gharama sana kibongobongo ila natumaini huko tunapoenda natumaini mambo yatabadilika
Kama ni mpenzi wa quality katika Tv kwa sasa Youtube ina support ku play hadi 8K kwahiyo kama utakuwa na Tv yako ambayo ni smart unaweza ku enjoy hapa kuangalia contents zenye 4K kupitia Youtube huu ni mfano wa 4K :-
Hilo ni game (Assasin Creed) lilikuwa linachezwa katika Pc ambayo imeunganishwa na Tv na kutestiwa utofauti kati ya 4K na 1080P, na kama unavyoona hapo utofauti unaonekana moja picha inaonesha details vizuri na nyingine ina kama blur hivi ila mwisho wa siku nashauri kama unaona hauna ulazima wa 4k just baki kwenye 1080P ila kama mpenzi wa teknolojia sana haya 4K ipo kwaajili yako.
4K AU 1080P AU 720P
Kwa sasa hata nchi zilizo endelea bado hawaja komaa katika matumizi ya 4K na ndio kwanza kwa mfano mwaka 2016 ndio deki zinazo play 4K zimetoka lakini zina Bei kubwa sana, kama 600,000 hivi na ukirudi kwa wale wazee wa consoles pia binafsi sidhani PS5 ikitoka au hiyo Xbox mpya itakayo toka kama ita support 4K na hata zikitoka bei yake itakuwa sio ya kitoto kwahiyo kati ya hivyo vitatu ningeshauri bora kukaa kwenye Tv yenye 1080P kwasababu mwisho wa siku utachukua 4K alaf itakuwa ni kituko kama hivi
Ukiona hapo hiyo ni Tv ambayo ni 4K na ndani video inayo play ni 720p ebu una nafasi inayobaki pembeni labda Tv ikiwa na uwezo wa kufanya Upscaling ndio ikuze hiyo video ienee kwa screen lakini ikikuza kumbuka Quality itapotea.
BAKI KWENYE 1080P ila kama una kiherehere kama mimi haya Nunua 4K for the future!
UKUBWA GANI WA TV UTAKUFAA
Nitarudi palepale kwamba ununuzi wa Tv ni chaguo la mtu binafsi ninacho kifanya ni kutoa ushauri tu ili mtu aweze kupata Tv nzuri ya kuangalia na ku enjoy
Kwa size za Tv nafahamu zipo nyingi mpaka inch 126 ila size ambayo itakayo mfanya mtu aenjoy kuangalia kionekanacho katika Tv ni kuanzia inch 40 kwenda juu, najua lazima utajifikiria sana ukubwa wa huo utapatikana kwa bei gani? kiukweli kwa Tv hizo kama LG au Samsung au SONY lazima upate kuanzia 1,000,000 mpaka milioni 1.5 mpaka milioni mbili lakini makampuni kama HISENSE wanatoa Tv zao zenye inch 40 kwa Tzsh 500,000 mpaka 700,000 inaweza kuwa kubwa lakini still ni bei nafuu ukiringanisha na hao wengine.
JE NI MUHIMU KUWA NA SMART TV
Smart Tvs binafsi naona sawa ni feature moja nzuri kwasababu unaweza uka browse google ukaingia YouTube na kadhalika lakini sidhani kama ukikosa utakuwa umekosa kitu kikubwa sana na kwa sababu hii basi makampuni ya Tv yanatumia nafasi hiyo kutuuzia Tv za Smart kwa bei ya juu sana, kwa mfano juzi nilienda Mlimani City katika store ya Game pale dada wa pale akaniambia Hio 1080p smart ni shilingi 1.9milioni na hiyo 1080P ambayo sio smart ni 1.2 milioni
sasa nikajiuliza kuwa na smart ndio laki saba nzima inaongezeka jamani? Kwahiyo kama unavyo ona wakiongeza kakitu kadogo tu basi bei wanaongeza pia like really bruuh?
Kama ingetokea nimesimamia zoezi la kutengeneza Tv ningeiita smart lakinu ningetoa vitu ambavyo havina umuhimu kivile kwa mfano SmartCast ni kitu kizuri sana katika Tv ambayo inakuwezesha kuplay kitu kwenye simu yako na ku display kule kwenye TV. kitu kama Wi-Fi ni muhimu sana kwenye Tv kwaajili ya kustream ingawa kwa bongo NETFLIX au HULU au AMAZON ambazo ni huduma za kustream zinazo onyesha Movies au Series etc baatimbaya kwa nchi kama Tanzania hatuna services hizo ila nimeona NETFLIX wamezindua Tanzania inapatikana ila embu imagine unastream episode moja ya Game Of Thrones ambayo ina dakika 50 alaf network zetu na bando zetu hizi khaa kwakweli inahitaji pumzi yakutosha na hela yakutosha, ila tunapoelekea natumai teknolojia itanyooka tu. kwahiyo tukiongelea smart Tv ufahamu kuwa utakacho enjoy ni Youtube labda na browser sasa ukiangalia hapo si wanatuuzia youtube na browser kwe laki saba ndugu zangu? Anyways mwisho wa siku ni mfuko wa mtu sooo.. yeah.
Kwakumaliza kabisa ndugu zangu mui napenda kutoa ushauri mkubwa kabisa wa kuangali sifa za Tv kabla hujanunua iwe mtumba au Mpya dukani usije ukanunua kitu ambacho ku enjoy huwezi kuna sifa nyingi sana ambazo zipo katika Tv zetu kwahiyo natumaini walau mambo haya machache yatakupa ufahamu na kufanya uamuzi mzuri katika kununua TV
cheers..
7 Comments
Ahsante kwakutufungua mzee mie binafsi umenisaidia kuchagua mzigo makini sana pamoja
ReplyDeleteMheshimiwa, Big Up kwa ushauri wenye afya, nadhani baada ya hapa watu tumefumbuliwa na mambo ya kufuata mkumbo wa kutumia fedha bila kujua nini ammana yake, umeliweka vizuri, binafsi nakushukuru na uendelee kubarikiwa
DeleteMusic system nayo vp ilike it
ReplyDeleteHii bro nimejifunza nilikuwa najua tu kuwa HD ni ibora wa Picha kumbe nimepata kitu hapa ndugu ubarikiwe
ReplyDeleteNimejifunza kitu hapa mkuu kwakua niko na mpango wa kununua tv nazani nitafanya maamuzi sahihi ubarikiwe sana mzee
ReplyDeletePamoja sana mkuu nimejifunza
ReplyDeleteHisense ni nzuri au magumashi
ReplyDelete