JE UNATAKA KUAGIZA SIMU EBAY AU AMAZON? NI RAHISI SANA SOMA HAPA (OFF TOPIC)

          
           
  UPDATE !!!!
   
       Kuna mabadiliko  tafadhali Soma hapa kwanza kabla hauja fika mbali, pia unaweza ukasoma post yote alaf ndo ukaja kusoma update hii ili uweze kuelewa vizuri.

  • Kwanzia tarehe 25 mwezi wa 12 Kampuni Ya stackry ilitangaza kuacha kusafirisha vitu vyote venye betri aina ya Li-ion Ndani Yake, (laptops , simu, nk) 
  • Kama utataka kununua vitu hvyo unaweza ukatumia njia mbadala kusafirishia  (kwa sasa unaweza ukatumia myUs ingawa  wao wanatumia Fedex na Dhl , na kama tunavyofahamu kule huwa wasumbufu sana kutoa mzigo wako,        
                Lakini pia kuna kampuni mpya ambayo pia nimeitumia inaitwa vykingship ambao unaweza kuwaceki kupitia website yao hapa www.vykingship.com ukiwa unaregister sehemu ya referrer code jaza (11722) ukijaza utaweza kupata punguzo la asilimia 10% ukiagiza mzigo kwa mara ya kwanza..
 Hawa vykingship wana ruhusu kusafirisha mizigo yenye betri lakini wana limit mizigo miwili yenye betri kwa mkupuo mmoja ambayo sio mbaya unaweza ukasafirisha simu yako nk.. kwa kutumia hawa jamaa, nimekuwa nikitumia hawa hawana tofauti kubwa sana na stackry  ni wazuri pia . bei zao ni cheap kuliko stackry na pia wana option ambayo unaweza ukachagua kutuma mzigo kama zawadi na kama unataka unaweza ukawaomba wafute invoice zote na waziandike unazo taka wewe ambayo ita cost $1.35 tu.
   
    Ni hayo tu natumaini nimeweza kuwasaidia wengi.




   Habari ndugu wasomaji wa blog hii, Leo kidogo tutakua off topic lakini najua kwa uwezo mmoja au mwingine tunaweza kusaidiana hapa" 

       Najua wengi wetu tunatamani sana kununua simu kutoka nchi za nje kwa sababu moja au nyingine kwa mfano, mimi niliacha kununua simu za smartphones hapa Nchini kutokana na sababu chache tu,


  • Ya kwanza ni Bei, hii ni sababu yangu binafsi  na ninapo zungumzia bei namaanisha kwa simu ambazo mimi binafsi ningependa kuwa nazo au kumiliki ambazo nyingi huwa ni bei kubwa sana 
  •  Kingine ni uniform, nadhani pia ni mimi binafsi napenda kuwa na simu ambayo watu wachache sana watakuwa nayo katika jamii inayo nizunguka  sio nakua kwenye gari alaf wote mmetoa simu ni kufanana kwa hali ya juu kwahiyo ninavo kuwa nanunua nje inasaidia kwasababu kuna baadhi ya makampuni hawa supply simu zao sehemu kama za nchini kwetu pengine ni kutokana na kutokuwa na soko au la wanasababu zao wenyewe.
  • Kingine ni kutaka umashuhuri tu wa kununua simu nje ingawa hapa nchini zinaweza kupatikana lol.. lakini pia inasemekana ukinunua simu ebay au amazon uwezekano wa kuuziwa simu feki ni mdogo kwa yule mzoefu lakini kama sio unaweza kupigwa kama kawa, sasa nitawafundisha hapa ili usitapeliwe sawa?
             
                                        JINSI YA KUANZA. 

             Kwanza kabisa wapendwa unatakiwa kuwa na vitu vichache vitakavyo kusaidia kufungua account na kuweza kulipia fedha zako  vitu hivyo ni kama ifuatavyo-:



  1. Account ya Benki (CRDB au BANC ABC)
       Ni lazima uwe na account kutoka katika benki nilizo zitaja hapo juu  sijaona na wala sina uhakika kama benki nyingine unaweza ukapewa account kama watakayo kupa hizo benki mbili tajwa, kiufupi ni kwamba mimi nimesha wahi kutumia benki zote mbili hapo juu na  kwa ushauri ni bora kufungua account katika benki ya BANC ABC kwa sababu CRDB wana milolongo mirefu mbali na hapo lazima ufungue account ya kawaida kwanza ndio pia wakufungulie  nyingine kwa ajili ya online purchase ila ukienda Banc Abc utawaambia wakupe kadi ya "visa cash card" ambayo ndiyo utakayo tumia katika shughuli za kununua vitu online, wako fasta tena ni bureee na hawana foleni mimi yangu nilichukulia pale Quality Center unahitaji uwe na kitambulisho cha mpiga kura au passportthen ni kitendo cha dk 10 tu mambo yote yanakuwa tayari.


    2. PayPal

   
    PayPal ndio njia pekee na salama ambayo itakusaidia kufanya transactions zako ziwe na usalama ili wale ma hackers wasiweze kukuibia, hii ni njia muhimu sana na ningewashauri wengi wajiunge nayo kwanza ingiwa unaweza kutumia kadi tu bila kujiunga na paypal lakin hata hivyo wauzaji wengi pia wa Ebay hawataki wateja wasio kuwa na PayPal ili kuzuia ule usumbufu. 
      Jinsi ya kujiunga na PayPal ni rahisi unacho takiwa kufanya ni kutembelea website yao (www.paypal.com) alaf uta bofya sehemu iliyo andikwa Sign Up for paypal alaf  utaletewa sehemu za kujaza


 
Sehemu inaonekana kama ilivyo katika picha hii
                      
     

        3. Account ya Ebay au Amazon, Sasa baada ya kupata hapo juu vitu hivyo nilivyo elezea unaweza ukaendelea na  kwenda kufungua account ya Ebay au amazon ambazo utaweza kuziifungua kwa kutembelea Website zao (www.ebay.com, na www.amazon.com)  kisha ufungue account mpya kama hauna account ambayo ni kitendo cha muda mfupi tu unajaza pale then mambo yatakua sawa, kama unavyo ona katika picha hapo chini.

                    

  Baada ya kufungua account Ebay unatakiwa kwenda kujaza ile account yako ya paypal ambayo tumefungua hapo juu ili kuweza ku link na Ebay, kufanya hivyo fuata maelekezo kama inavyo onesha katika picha hapa chini




1. Baada ya kufungua account itakuleta sehemu hii kama unavyo ona hapo juu katika picha alaf bofya katika sehemu imeandikwa "Account" (nimezungushia wino mwekundu)







2. Kisha utachagua sehemu iliyo andikwa "PayPal Account" upande wa kushoto (nimezngushia wino mwekundu)





3.Account yakwangu nime link tayari ila kama ni mara ya kwanza utaona wamekwambia "link your paypal"   katika hiyo sehemu niliyo zungushia wino mwekundu then utajaza payapal yako ambayo itakua ni email address uliyo jaza katika paypal na password yake.




4. ukisha ilink account yako sasa  unatakiwa kujaza address yako ambayo ukinunua mzigo wata utuma katika address  hiyo, kama unavyo ona utachagua sehemu hiyo kushoto iliyo andikwa Addresses (nimezngushia wino mwekundu). Ukiangalia kulia utaona wameandika "change" mara tatu hii ni kwa sababu tayari nilisha jaza ila kwako kama ni mara ya kwanza itakuambia create  ambapo ndipo unapotakiwa ku select hapo ili kujaza address zako.


 



5. Ukisha select  Create itakuleta katika kujaza kama unavyo ona hapo chini sasa katika eneo hili kuna maelezo menine ambayo tunatakiwa kufahamshana,




      Kabla hatujafika namba 7 swala la Address ni muhimu na ndilo linalo changanya watu wengi mno, mara nyingi wauzaji wa ebay hawasafirishi kwenda nchi za africa huwa wana fanya kuuza palepale US.

     Kwahiyo hapa unacho takiwa kufanya ni  kufungua account katika kampuni ambayo inafanya kazi  ya kusafirisha bidhaa ambazo zimenunuliwa  kutoka marekani na wana zifoward kwenda nchi nyingine, kwa maana hiyo mimi nimetumia makampuni tofauti kama vile MyUs, Aftership, shipto na Stackry na kwakweli kampuni ambayo nimevutiwa nayo ni Stackry  na ndiyo ninayo itumia mpaka sasa ila nimeona watu wakiisifia myUs ila binafsi sijawapenda na service zao kama marobot kwahiyo nisinge washauri watu watumie, unaweza kutembelea website hii ambayo watu wanaenda kutoa maoni kutokana na vile walivyo hudumiwa unaweza kutembelea  kwa kubofya hapa www.sitejabber.com  
    1. Ukitembelea "www.stackry.com " website yao itaonekana kama hapo chini kisha chagua sehemu iliyo andikwa "sign up"  upande wa kulia nimezungishia wino mwekundu.
    


2. kujiunga ni kama unavyo ona hapo chini  utajaza kilakitu hapo  ila sehemu ya chini kabisa iliyo andikwa referral code unaweza kutumia code ya 78660 ambayo ukijaza utapunguziwa $10 ukitaka kulipia hela ya usafirishaji wa mzigo wako   au tumia linki hii ikupeleke moja kwa moja kupata punguzo hilo  https://www.stackry.com/register?referral=78660



3.ukisha fungua account
ya stackry uki login utaonyeshwa address yako ya USA, na hiyo ndiyo utatumia katika  ile sehemu ya kujaza address kwenye account yako ya Ebay kwahiyo ukinunua kitu katika Ebay wanatuma kwa hiyo  address ambayo hawa watu wa stackry watakuwa wamekupatia then mzigo ukifika wanaufoward Tanzania. 

Address yako unaweza kuiona kama unavyo ona katika picha hapa chini upande wa kulia
ukisha log in itaonekana kama hivi
 
4. Baada ya hapo kinacho fuata ni kwenda Ebay na ku add account ya stackry ambayo tumesha iifungua na tumesha pewa address yetu, 

   
    Hii ni address yangu ambayo tayari nimesha iadd kwenye account yangu ya Ebay kwahiyo inanoneka kama unavyo ona katika picha




  Hapa ndipo unapo jaza ile address yako uliyopewa kule stackry  ili iwe address ambayo watakutumia mizigo ili iende kule then wa foward kuja nchini kwetu.




            Kwahiyo mabibi na mabwana ukisha maliza hatua hizo juu nilizozitaja uanaweza ukaanza kununua vitu vyako, sasa kuna mambo muhimu unatakiwa kuyafahamu kamaifuatavyo,
  
    USAFIRSHAJI
         Stackry wana njia nyingi ambazo wanatumia kukusafirishia mzigo wako  nia hizo ni kama ifuatavyo 


    
  Ninge washauri watu wengi kwamba wasijaribu kutumia FEDEX au DHL  labda tu kama mzigo wako utakao nunua ni wa bei ghari mf, TV nk.. ila kwa laptop sijui simu na vinginevyo vidogo ningeshauri mtu atumie USPS au Global Mail, mii nimeshawahi kutumia zote ndio maana nikatoa shauri  na kama una mzigo mdogo lakini una thamani ningeshauri utumie USPS ambao ndani ya siku 5 mpaka 8 mzigo unakua umesha fika, ila kwa wale wa vitu vidogo havina thamani sana unaweza tumia GLOBAL MAIL. 

      GHARAMA

     Gharama ya kusafirishia mizigo utrakayo iagiza kutoka Ebay kwenda Stackry  mara nyingi huwa ni free, gharama ya kusafirishia mzigo huwa inakuja pale unapotaka kuutoa Stackry kuja Tanzania ambapo kama nilivyo waoyesha njia hapo juu kila njia ina bei yake alaf bei hutokana na Ukubwa na uzito wa mzigo wako, kwa mf.. niliagiza simu mbili nikalipia $54 kusafirisha kuja Tz kwa kutumia njia ya GLOBAL MAIL  na mzigo ukafika ndani ya siku 15 ila kulikuwa na njia nyingine ambazo pia  zingekua za fasta zaidi ila tu gharama yake ilikua ni kubwa




     HUDUMA
  Huduma zao stackry ni nzuri mno na nimekuwa nao kwa mwaka wa 2 mpaka sasa na sijawai kupata shida nao hata, ukiagiza mzigo ukifika kwao wanakupa ruhusa ya kukutunzia mzigo kwa muda wa siku 45 bure kwahiyo kama ulinunua mzigo haujapata pesa ya kusafirishia kwa siku 45 hizo una uwezo wa kupata pesa na ukakamilisha mambo yako.


  Basi kama ilivyo kawaida ya blog hii ningependa kutoa shukran kwa kusoma na natumai umeweza kuelewa  na kuondoa uwoga wa kuagiza vitu  kisa wezi  wa mtandao, Asanteni sana na  karibuni kwa post nyingine 



Pia unaruhusiwa  kuuliza kama hauja elewa kitu katika post hii 

Cheers...

Aq

Post a Comment

58 Comments

  1. shukran kwa farasa safi.nilikuwa naomba ufafanuzi kidigo,kwa mfano nimenunua laptop ebay hapo Us,nataka kutumia DHL gharama zake had ifike hapa nishingapi?
    Je,mzigo ukifika hapa tz nitakatwa ushuru?? (kama ni laptop).shukran

    ReplyDelete
    Replies
    1. habari asante sana kwa kutembelea blog hii, sasa kiufupi gharama zake siwezi kukadiria kutokana na kila laptop ina uzito, upana na urefu tofauti. ila ninaweza kukupa mfano mimi nilisha wahi kuagiza playstation 3 ambayo ilikuwa inagharimu $250 nilitumia DHL kusafirisha na walinichaji Tzsh 190,000 kwa usafiri pekee.. kwa upande wa kodi kwa laptop ni lazima ulipe ingawa kuna watu huwa wanasema a kama utasema ni ya matumizi ya shule basi hauta tozwa kodi, wangu binafsi sijawahi hivyo. Na kodi watakutoza kutokana na gharama ulizo nunulia mzigo na pia ni jinsi gan utaweza kujielezea. Asante atumaini nimejibu swali lako.

      Delete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Habari, Asante sana kwa maoni tumesha fikiria kufanya hicho kitu na hivi karibuni tutafungua channel nakuanza kupost video kwa muongozo mzuri zaidi Karibu sana.

      Delete
    2. This comment has been removed by the author.

      Delete
    3. Habari, asante kwa kutembelea blog hii. sasa ndugu kuagiza kitu south ningependa kufahamu ni kitu gani ili walau niweze kukuambia range ya kodi ingawa kule customs kuna charges nyingine unaweza kukutana nazo na bei nitakayo kuambia inaweza kupanda au kushuka. karibu sana.

      Delete
  3. Ningependa kufahamu ni wapi tanzania mzigo unafikia namaanisha Posta,ofc za campuni ama mf iyo global mail unaupokelea wapi...vp usalama wa mzigo pindi ufikapo ktk mikon ya wafanya kazi tanzania hususan posta na bandari.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana kwa kutembelea blog hii kwa kujibu swali lako naweza kusema inategemea ni njia gan utatumia kisafirishia mizigo yako, mfano kwa njia ya global mail au posta(USPS) mzigo utapelekwa posta mpya pale na ndipo utakapoenda kuchukulia mzigo wako. kama ukitumia fedex au dhl au ups utakwenda airport kule kuchukua mzigo wako na kuna usumbufu na gharama za hali ya juu kwa upande wa kodi, huwa siwashauri watu wasitumie hizo njia labda tu kama wanasafirisha mzigo mkubwa kama vile tv na kadharika, na swala la usalama mizigo posta pale inaingia kwa usalama zaidi wala hakuna tabia zile za kuiba kama zaman sikuhizi mzigo utaupata na ni muhimu ununue mzigo unaotoa tracking number ili uwe una utrack kwahiyo ni ngumu kupotea wala usijali mi nna uzoefu wa miaka mi 5 hivi tangu nianze kuagiza na mara nyingi natumia njia ya posta.

      Delete
  4. ningependa kujua
    1. cost inayokatwa na benk kwa kila transaction au n free pia
    2.kama kwa watu wa mikoa mingine tunaandika anuan zetu za mikoan au mpaka uwe na anuan ya dar

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama upo mkoani ni vizuri kwanza ukaulize pale ofisi yako ya posta kama watakuletea ingawa najua wanaweza kuku letea mzigo wako ila ni vizuri kwenda ukafahamu taratibu zao kwanza, swala la fee kwa BanC Abc ni free kwa kila ufanyapo transacrion hawakukati sijajua benki nyinginezo kama nao wanafanya free

      Karibu sana.

      Delete
  5. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  6. Asante kwa Elimu na kazi nzuri ya kutuelimisha. Mimi nataka kuagiza nguo za watoto kama 23 hv kwa ajili ya biashara nataka kuzinunua China kupitia mtandao wa Ali express. Wauzaji wamesema wao watautuma bure yaani free shipping kwa njia ya posta(hongkong post) swali nauliza. Je mzigo ukishafika Posta Tanzania nitatakiwa kulipa ushuru au ni free?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sina uzoefu sana na aliexpress ila kwa kupitia posta (kama utaupata) wanasheria zao wenyew nadhani mzigo ukizidi ujazo fulani (kilo kadhaa) basi ni lazima ulipe ushuru na pia unatakiwa uwe una maelezo mazuri kuhusu aina ya mzigo kama ni wa biashara au wa matumizi binafsi, ningeshauri useme ni wa binafsi kwani ukisema wa biashara utatozwa kodi kubwa.. natumaini nimekusaidia hapa.

      Delete
    2. kuna mabadiliko nime post juu kabisa ya post hii(Update) ningependa upitie usome Asante.

      Delete
  7. Nimependa kwa kweli kwa elimu hii' ni very useful... Hongera zako

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shukrani sana na asante kwa kutembelea blog hii

      Delete
  8. pole sana kwa kazi ya kuelimksha umma,,ninaswali kama ifuatavyo...
    Nilikuwa na mpango wa kuagiza smart tv inch kama 46 hadi 50 us,vipi naweza tumia njia gani, na kodi itakuwa kiasi gani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Samahani sana kwa kuchelewa kujibu swali lako, Sasa kwa Tv kama unataka kununua naweza lakini kama ni inch 50 hauta tumia kampuni ya Stackry kwasababu wao hawasafirishi mizigo mikubwa sana, kwa hiyo itakubidi utumie MyUs ambao wao sasa.. wanatumia njia ya fedex au Dhl na kwa mfano dhahir kabisa mimi nilisha nunua inch 50 kwa usd 320. lakini ulivyo fika hapa ilibidi nilipie gharama takriban laki 6 za kila kitu kuutoa mzigo pale airport customs, tambua kuna watu wa TBS, sijui ushuru na wengineo kwahiyo gharama hua zinakua kubwa, lakini pia inategemea na declared value utakayo iweka katika mzigo wako. kwahiyo ndio unaweza ila utegemee gharama nyingi za kutoa mzigo kwasababu hauta uchukua kupitia posta

      Delete
  9. Msaada wako ni mkubwa sana, bila kujua njia hizi za kampuni za usafirishaji hatutoweza kununua chochote ebay...thank you ,,umetusaidia sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. kuna mabadiliko nime post juu kabisa ya post hii(Update) ningependa upitie usome Asante.

      Delete
  10. ningependa kujua kama kuna kodi inatozwa ili kuchukua simu uliyoagiza kwa USPS (ukiachana na shipping fee ), na kwa makadilio inaweza kuwa kiasi gani ?

    ReplyDelete
    Replies
    1. yes kodi ni lazima utozwe, ku kadilia ni kwamba inategemea na gharama ya simu ila kama itagonga kwenye 250,000 mpaka 300,000 tzsh unaweza kulipia 60000tzsh kama kodi, ila siwezi kadiria exactly sababu rate pia ina badilika kila siku
      karibu sana

      Delete
    2. kuna mabadiliko nime post juu kabisa ya post hii(Update) ningependa upitie usome Asante.

      Delete
  11. Article nzuri sana. Inaniongoza kwenye mambo yote niliyotaka kujua. Nina jambo ningeomba nieleweshwe kidogo. niko mbioni kuagiza camera na equipments chache ebay ila issue ya kodi inanipa changamoto kulingana na fixed budget yangu. niliwahi kuambiwa kuna njia unaweza kutumia usitozwe kodi, kwa mfano, ukiji commit kuwa wewe ni mfanya biashara utatozwa, na kama ni vitu binafsi hautozwi, je hili lina ukweli? Na kama halina ukweli, je kuna njia za mimi kufikisha vitu vyangu bila kodi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana kwa kutembelea blog hii, kiukweli swala la kodi ni vile wewe utakavyoweza kuongea na swala la kusema eti vitu binafsi kikawaida inatakiwa usitozwe kwa baadhi ya vitu, ila wale jamaa pale wata kubana kila upande mpaka mwisho wa siku utatoa tu, yani haikwepeki lazima utozwe ingawa inategemea na utakae mkuta na vile utatoa maelezo yako..
      kama utaagiza kamera inategemea na gharama ya kamera na ukubwa wake kama ni ya gharama andaa tu pesa za kodi.

      Delete
    2. Asante sana kwa feedback mkuu

      Delete
    3. Na issue nyingine ya mwisho ndugu, unaweza kujua ni asilimia ngapi ya total cost ndo inatumika kama tax. Au total tax percentage ni ngapi? Najua VAT ni 18% sasa sijui kama kuna tozo zingine zinaongezeka apo kama import duty au vitu kama ivo. Atleast niweze kuwa na picha ni sh ngapi nijiandae nayo

      Delete
    4. Shukrani sana, Kama siokosei ni nadhani ni 25% sijafahamu kama kunamabadiliko kwasababu mara ya mwisho kuagiza mzigo ni mwezi wa pili mwaka huu, inaweza ikawa chini yake au ikaongezeka

      Delete
    5. Shukrani sana. Page yako na feedback zako ni msaada mkubwa mno. Asante

      Delete
  12. Aksante sana ndugu. umetatua tatizo langu la muda mrefu sana. nina swali moja. nimenunua vitu toka ebay. vimeshafika stackry na wameshanitumia. nimetumia Global mail kwa sababu nioption yenye bei nzuri. sasa kwa mkoani Mbeya itanifikia kirahisi kweli? Global mail vitu vinafikia posta au airport? Je wanakupigia simu vikishafika au ni kwa njia gani utajua vitu vyako vimefika? Aksante

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwa global mail mzigo utatakiwa uufate posta kwasababu ukitoka stackruly wana wapa dhl alaf ukifika tanzania dhl wanawakabidhi posta kwahiyo utatakiwa uende kule na kikubwa usisubiri upigiwe uwe tu una track mzigo wako mara kwa mara nadhani ndani ya siku 7 au 8 utakuwa umefika kama uko mbeya inabidi uwai mapema posta uwape taarifa ili ujue watakusaidiaje kama utaletewa au vip

      Delete
  13. kwa global mail mzigo utatakiwa uufate posta kwasababu ukitoka stackruly wana wapa dhl alaf ukifika tanzania dhl wanawakabidhi posta kwahiyo utatakiwa uende kule na kikubwa usisubiri upigiwe uwe tu una track mzigo wako mara kwa mara nadhani ndani ya siku 7 au 8 utakuwa umefika kama uko mbeya inabidi uwai mapema posta uwape taarifa ili ujue watakusaidiaje kama utaletewa au vip

    ReplyDelete
  14. asante sana kwa herimu yako
    kwamfaano mm nataka niagize mojakwa moja toka ebay.bilakutumia izo kampun za kusafirisha mizigo.nikanunua toka kwa muuzaji anaetuma international shiping.inawezekana?

    ReplyDelete
    Replies
    1. unaweza kuagiza moja kwa moja lakini wauzaji wengi katika ebay hawasafirishi moja kwa moja hua wanaishia Us na nchi za jirani lakini wapo ambao wanasafirisha moja kwa moja, kikubwa ni wewe kumfuata muuzaji na kumtumia meseji private umuulize kama ataweza kukutumia moja kwa moja kama mtakubaliana then unaweza kufanya hivyo ila uwe muangalifu hakikisha kama anahitaji malipo basi mfanye katika ebay humo humo na sio sehemu nyingine

      Delete
    2. kuna mabadiliko nime post juu kabisa ya post hii(Update) ningependa upitie usome Asante.

      Delete
  15. Nimepata majibu ya maswal yote kwa wakat mmoja asante sana mkuu kwa mada hii ,,nitakurafuta zaid nitakapokwama

    ReplyDelete
    Replies
    1. kuna mabadiliko nime post juu kabisa ya post hii(Update) ningependa upitie usome Asante.

      Delete
  16. Hii Elimu nzuri sana, naomba kujua kama hauna Box adress Posta Mzigo Kuupata inawezekana?

    ReplyDelete
    Replies
    1. kuna mabadiliko nime post juu kabisa ya post hii(Update) ningependa upitie usome , kujibu swal lako ni ndio inawezekana sio lazima uwe na boksi kwasababu hata ukiwa nalo utapigiwa simu ukajibu maswali customs, kikubwa usisahau kuandika namba ya simu .

      Delete
  17. Habari yako mkuu samahan nilikua naomba ufanunuz kuhusu kufungua paypal account... Kuna sehemu wanasema ni add casaasasa hapnanajaza card gan na vp kama sina card naweza tumia njia nyingine?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Habari kwa baat nzuri kuna video nimefanya inaelezea vizuri...
      link hii apa.

      https://youtu.be/C-EOr5ziLJM

      Delete
  18. Kaka kuna kitu kina nitatiza njinsi ya kuunganisha stackry na account yang ya Amazon hapo bado sijaelewa kaka

    ReplyDelete
    Replies
    1. ingia kwenye link hii kaangalie video part 1 mpaka 4 nimeelezea kiuref https://youtu.be/V6Q0Eb5GX8U

      Delete
  19. kaka hongera kwanza kwa kutupa elimu ila bado tuanitaji elimu zaid kama ulivyosema kuwa utatuwekea video ya jinsi ya kununua vitu kwa njia ya mnada

    ReplyDelete
    Replies
    1. ingia kwenye linki hii, videoipo hewani kaitizame ujifunze zaid
      https://youtu.be/V6Q0Eb5GX8U

      Delete
  20. Pole kwa majukumu kaka. Samahani nilikua nasikiliza video zako za youtube kuhusu namna nzuri ya kuagiza vitu online. Ila kuna changamoto nilikua napata kwenye amazon ambayo pamoja na kusikiliza kwa makini video zako au kusoma blog yako bado sijaisolve. Kule amazoni nilisearch product na ikaonyesha free internal shipping na wakaonyesha kwamba mzigo unaweza kuwa shipped to tanzania. Ila cha kushangaza nikiandika anuani yangu ya posta kule amazoni wanajibu kwamba mzigo husika hauwezi kuwa shippped kwenye hilo sanduku la posta. Nilikua naomba msaada kama kuna baadhi ya anuani za posta tanzania zinatambulika na amazoni au naomba unielekeze anuani gani napaswa kuijaza ili niweze kuupata huo mzigo tanzania kwa kutumia hiyo free international shipping.

    ReplyDelete
  21. Pole Na Kazi Mkuu Naomba Kujua Baada Ya Kufanya Yote Hata Natambulika Vipi Na Hao Stackry Kwamba Huu Mzigo Ufowardiwe Tanzania....

    Na Naupata Vipi Ukishafika Nchini

    ReplyDelete
  22. Asante sana kwa maelezo mazuri sana. Je ni muhimu kuanza kuregister stackry ili address watakayokupa ndo hiyo uitumie kusign in paypal? Na Je stackry wanaweza kupokea mizigo nje ya Marekani na kunitumia mimi? Mfano: nataka kununua bidhaa alibaba na supplier anaonekana yuko China, mzigo wangu nitaupata kweli?!!

    ReplyDelete
  23. Kongole kaka mwenyezimungu akuzidishie elimu zaidi yenyemanufaakwajamii

    ReplyDelete
  24. Nimejaribu ku update lakin sijafanikiwa

    ReplyDelete
  25. Nimejaribu ku update lakin sijafanikiwa

    ReplyDelete
  26. Nimejaribu ku updatelakini sijafanikiwa

    ReplyDelete
  27. Mkuu vip nahitaji kuaagiza vifaa vya studio kwa mf. Microphone na sound card

    ReplyDelete